IJUMAA Newspaper REPORTS:- Kile kilio cha muda mrefu cha wasanii kulalamikia kulizwa na mdosi katika usambazaji wa kazi zao kinaelekea kutatuliwa, na watatuzi si wengine bali ni vijana wadogo ambao ndiyo wakurugenzi wa site ya wajanja ya G5 Click. Blogu hiyo ambayo ni namba moja nchini kuanzia layout, ripoti za muziki wa kiwanja na ndani ya nchi, wametangaza kuwa hivi sasa wanajipanga ili waweze kusambaza kazi za wasanii online.
Madogo wanaounda G5 ni Mustapha Suleiman, Ombeni Phiri, Desy Ernest na Nelson Kisanga ambao kupitia ubunifu wao, wameweza kuitengeneza G5click.com ambayo inavuma anga za kimataifa kiasi cha wengine kuifananisha na Facebook. Usipime! Akigonga matamshi kwa niaba ya wenzake, Mustapha alisema: “Tunajipanga kwa ajili ya kutambulisha njia mpya ya kutangaza, kusambaza na kuuza kazi za wasanii ili
waondokane na kilio plus lawama kwa mdosi.” Mbali na hilo, mzozo wa XXL Teen extraAwards unaendelea na G5 Click inawania tuzo ya Music Website of the Year ambayo nicategory iliyopewa herufi D. Katika category hiyo, vichwa kadhaa vimesimamishwa, DJ Choka (D2), Bongo5 (D3), DJ Fetty (D4), Babkubwa (D5) na G5 Click (D1).

Jinsi ya kupiga kura kwenye category hiyo, unaandika SMS yenye neno TN unaacha nafasi ikifuatiwa na namba yake ya utambulisho (code) halafu unatuma kwenda 15551.


Unaikubali G5? Gonga SMS yenye
maandishi, TN D1 halafu unaitupa kwenda
namba 15551. Pia unaweza kutembelea Nipe5.


Leave a Reply